♠ Posted by Unknown at 12:17
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania, Luis Figo,
WACHEZAJI wa
zamani wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania, Luis Figo, Michael Owen
pamoja na Cristian Karembeu, tayari wametua nchini kwa ajili ya mchezo
wa kirafiki utakaopigwakesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya kikosi maalum cha nyota wa Tanzania, Tanzania Eleven.
Kikosi kizima cha wakongwe, kimetua nchini na ndege ya Shirika la Emirates tayari kwa mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.Mratibu wa ziara hiyo, Denis Ssebo, amesema kuwa Figo, Owen na Karembeu tayari wameingia nchini huku kikosi kilichobakia kikitarajiwa kuingia leo.
“Tunashukuru Mungu maandalizi yanaenda vizuri na jana (juzi) usiku tumewapokea Figo, Karembeu na Owen ambao wote waliwahi kuichezea Madrid katika vipindi tofauti.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania,Michael Owen.
“Tunategemea kupokea kikosi kilichobakia ambacho kwanza kitatua Dubai
na baadaye kuingia nchini na kitaelekea Hoteli ya Bahari Beach, jioni
kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa,” alisema Ssebo.Pia mchezaji mwingine wa Stars anayeishi nchini Uingereza, Athumani China, alitua jana na kuanza mazoezi moja kwa moja kwa ajili ya mechi hiyo kwenye Uwanja wa Karume akiwa na wakongwe wenzake wa Tanzania.
Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Tanzania Eleven, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mechi hiyo. “Nafurahi kuona mahudhurio mazuri ya wachezaji wote walioitwa,” alisema Mkwasa.
Posted by Mr.Prime on August 22


0 comments:
Chapisha Maoni