♠ Posted by Unknown at 12:14
Kocha mkuu wa Simba Mzambia, Patrick Phiri.
MAKOCHA wa
klabu kongwe na pinzani za Simba na Yanga, keshokutwa Jumapili kila
mmoja atatumiamuda wake kwa ajili ya kusoma mbinu za mwenzake ndani ya uwanja mmoja.
Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa makocha hao kukutana kwenye uwanja mmoja ambapo Yanga inanolewa na Mbrazili, Marcio Maximo huku Simba ikifundishwa na Mzambia, Patrick Phiri.
Timu zote zinatarajiwa kucheza mechi kwa wakati tofauti kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na msimu mpya wa 2014/15 unaotarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu.
Yanga itakuwa ikicheza mechi ya pili tangu ilipoanza kuweka kambi kisiwani hapa, wakati Phiri atakuwa akiiongoza Simba kwa mara ya kwanza tangu amrithi Mcroatia, Zdravko Logarusic.
Phiri ameliambia gazeti hii kuwa mechi yake itakuwa ni dhidi ya Chipukizi ya Zanzibar inayoshiriki Ligi Daraja Kwanza visiwani hapa.
Kocha mkuu wa Yanga Mbrazili, Marcio Maximo.
“Timu yangu inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kirafiki Jumapili hii
kwenye Uwanja wa Amaan, mechi itachezwa usiku,” alisema Phiri.Wakati kocha huyo akisema hivyo, Yanga nao wamepanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhid ya timu mojawapo inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar mapema siku hiyohiyo.
Taarifa kutoka ndani ya benchi la ufundi la Yanga ni kuwa, mchezo huo ni sehemu ya mpango wa kucheza mechi tatu za kirafiki kwa muda wote watakaokuwa kambini, ambapo walianza na Chipukizi ya Pemba, jana.
“Kocha amehitaji michezo mitatu ya kirafiki, tunatarajia kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Chipukizi leo (jana), baada ya hapo Jumamosi tutaelekea Zanzibar, tutacheza mechi mbili,” alisema mtoa taarifa.
Posted by Mr,Prime on August 22, 2014




0 comments:
Chapisha Maoni