♠ Posted by Unknown at 21:42
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo.
KOCHA wa
Yanga, Marcio Maximo, amepewa ripoti kamili kuwa timu yake itafungua
msimu wa 2014/15 kwa kukipiga na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Bara,
ambapo ameambiwa kuwa hao ni wapinzani wao wagumu na wameisumbua Yanga
kwa miaka miwili iliyopita.Maximo ameipokea ripoti hiyo kwa mikono miwili na kusema kuwa, atauvunja mwiko huo wa kuwa Mtibwa ni wagumu na wameonekana kuwa kiboko kwa Yanga kila walipokutana hivi karibuni.
Kocha huyo raia wa Brazil amesema wazi kuwa mechi hiyo ya Septemba 20, kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, itakuwa ya kawaida kwake na lazima Mtibwa wakae siku hiyo.
Akizungumza na Championi Jumamosi katika mahojiano maalum kwenye kambi ya timu hiyo kisiwani Pemba, jana, Maximo alionyesha kujiamini na kusisitiza kuwa, suala la kufungwa katika mechi hiyo kwake halipo, hata kama ni mechi ya ugenini.
Bosi huyo wa zamani wa Taifa Stars ameweka wazi kuwa, anamjua vizuri Kocha Mkuu wa Mtibwa, Mecky Maxime kwa kuwa amewahi kumfundisha katika timu ya taifa na siyo mgeni kwake.
“Kati ya vitu ambavyo ninaviweza ni kuifunga Mtibwa Sugar, nimepata taarifa za timu hiyo kuwa ngumu kila inapokutana na Yanga katika misimu mitatu mfululizo.
“Mimi nimepanga kumaliza mwiko huo, sitakubali kufungwa na Mtibwa Sugar katika msimu ujao wa ligi kuu, hao makocha waliowafunga iwe mwisho na siyo kwangu.
“Ninajua haitakuwa mechi nyepesi, itakuwa ngumu kutokana na ubora wa timu hiyo, isitoshe kocha wao niliwahi kumfundisha,” alisema Maximo akionyesha kujiamini.
Rekodi zinaonyesha kuwa, katika mechi nne za misimu miwili iliyopita baina ya timu hizo kwenye Ligi Kuu Bara, Yanga imeshinda moja, imefungwa moja na sare mbili.
Yanga Vs Mtibwa Sugar misimu miwili iliyopita:
Septemba 19, 2012: Mtibwa 3-0 Yanga, wafungaji wakiwa ni Hussein Javu mawili na Dickson Daudi, Februari 2, 2013: Yanga 1-1 Mtibwa, wafungaji ni Hamis Kiiza kwa Yanga na Shaban Kisiga.
Oktoba 5, 2013: Yanga 2-0 Mtibwa, wafungaji ni Didier Kavumbagu na Mrisho Ngassa, Machi 5, 2014 Mtibwa 0-0 Yanga.
Posted byMr.Prime on August 24, 2014



0 comments:
Chapisha Maoni