♠ Posted by Unknown at 16:16
Na Gladness Mallya
BAADA ya hivi karibuni Katibu wa Bongo Movie Unity, William Mtitu kutangaza
kujiuzulu na kuiacha nafasi hiyo wazi, Katibu Msaidizi, Devota Mbaga amefunguka kuwa anajiandaa kushika nafasi na kwamba kujiuzulu kwake hakusaidii chochote kwani wanachama wanahitaji fedha.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Devota Mbaga.
Akistorisha na paparazi wetu Devota alisema hatua ya Mtitu kujiuzulu
haisaidii kitu, wanachama wanahitaji fedha ambazo wamekula kwani
alitangaza kujiuzulu baada ya kuambiwa aweke mezani fedha walizokula.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects, William J. Mtitu akitabasamu ndani ya studio za Global TV Online.
“Najiandaa kushika wadhifa huo kufuatia Mtitu kuachia nafasi baada ya
kuambiwa aweke mezani fedha walizokula, amefanya hivyo, ili aonekane
msafi arudishe fedha au aje awaombe msamaha wanachama,” alisema Devota.Posted by Mr.Primeon August 22, 2014

0 comments:
Chapisha Maoni