♠ Posted by Unknown at 02:51

Kocha wa Simba, Patrick Phiri
KAMA Simba hii ikikamilika mmekwisha. Kocha wa Simba, Patrick Phiri
ameutaka uongozi wa klabu hiyo kufanya usajili wa wachezaji sita wenye
uwezo wa juu huku straika wa Mtibwa Sugar, Ame Ally na beki Hamis Kessy
wakiwa chaguo lake la kwanza.
Mbali na mastaa hao wa Mtibwa,uongozi umetangaza kumnunua winga wa
Yanga, Simon Msuva. Phiri alisema endapo uongozi utampa nafasi ya
kupendekeza usajili wa wachezaji wa kigeni atawaletea mastaa wa maana
kutoka Zambia.
Phiri aliingia matatani kwenye kikosi hicho baada ya Simba kucheza mechi
sita bila kupata ushindi jambo ambalo amesema hataki litokee tena
Msimbazi. Simba ilishinda mchezo mmoja pekee katika mechi saba za msimu
huu na kutoka sare mara sita.
Kocha huyo alitumia muda wa siku mbili akiwa amejifungia kwenye moja ya
nyumba tulivu eneo la Kunduchi, Dar es Salaam kuandaa ripoti ya mechi
saba za msimu huu na kutoa mapendekezo kadhaa ya marekebisho na
kuikabidhi kwa viongozi juzi Jumatano mchana na jana Alhamisi alitarajia
kukutana na viongozi wake kwa ajili ya kuijadili.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’, alisema
anahitaji winga mmoja, kiungo mchezeshaji mmoja na straika wa kati mmoja
ili kuifanya safu yake ya ushambuliaji kuwa ya kutisha zaidi nchini.
Imefahamika kuwa licha ya kocha huyo kuruhusiwa kupendekeza wachezaji
kutoka Yanga na Azam, ameelekeza nguvu kubwa kuwanasa mastaa kadhaa
kutoka kwenye kikosi cha Mtibwa wakiwemo straika Ame na Kessy.
“Nataka kikosi kifanyiwe marekebisho kadhaa hususani kwenye eneo la beki
na ushambuliaji. Kwa kifupi ni kwamba nahitaji winga wa kulia mmoja,
kiungo mchezeshaji mmoja na straika wa kati mmoja, nahitaji pia beki wa
kulia mmoja na beki wa kati mmoja,” alisema Phiri na kubainisha kuwa
anahitaji wachezaji sita pekee.
“Kuna wachezaji wawili wa Mtibwa nimewapendekeza, sema siwafahamu majina
hivyo nimeandika namba zao, kuhusu wachezaji kutoka nje nimeliacha hilo
kwa viongozi lakini kama wataniruhusu naweza kuja na wachezaji wazuri
kutoka Zambia,” anaeleza Phiri na kusema kuwa atakwenda kwao kwa
mapumziko mwishoni mwa wiki hii.
Akieleza sababu za kuwapiga chini mastaa wa Yanga kwenye mapendekezo
yake hayo, Phiri alisema bado hajaona mchezaji wa klabu hiyo mwenye
kiwango cha juu wa kuweza kuisaidia Simba msimu huu hivyo ni vyema
akasajili kutoka kwenye klabu nyingine ingawa tayari waajiri wake
wametangaza rasmi kufukuzia saini ya Simon Msuva.
Taarifa za ndani kutoka Simba pia zinaeleza kuwa kuna uwezekano wa klabu
hiyo kumrejesha beki Shomary Kapombe, ambaye yuko Azam lakini kwa
makubaliano ya kubadilishana na mmoja wa mastraika wa timu hiyo jambo
ambalo bado linajadiliwa.
Wakati huo huo, Phiri alisema anafahamu kuwa amebakisha mtihani mmoja
ili aweze kuendelea na kibarua chake Simba na kuutaja mtihani huo kuwa
ni kuifunga Yanga kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe, Desemba mwaka huu.
“Nafahamu kilichompata kocha wa Yanga (Ernest Brandts) msimu uliopita,
nahafamu kuwa alifukuzwa baada ya kufungwa kwenye mechi hiyo, ni lazima
nishinde ili kujiweka pazuri.

0 comments:
Chapisha Maoni