RAIS KIKWETE AKUTANA NA BIBI YAKE RAIS OBAMA WA MAREKANI, JIJINI NAIROBI LEO

♠ Posted by Unknown at 06:55

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Bibi yake Rais wa Marekani, Mh. Barack Obama, Mama Sarah Obama walipokutana leo kwenye hoteli ya Villa Rosa Kempiski jijini Nairobi, Kenya, wakati Rais Kikwete akijiandaa kurejea nchini. Mama Sarah Obama anatarajia kuzindua taasisi ya kusaidia elimu kijijini Kogelo nchini Kenya, alikozaliwa Baba yake na Rais Obama wa Marekani itakayofahamika kama (Sarah Obama foundation) ambapo atajenga shule kuanzia za awali mpaka sekondari. Rais kikwete sasa hivi yuko mjini Kondoa kuendelea na ziara yake ya Mkoa wa Dodoma

1 comments:

I am not impressed. Vazi la Kikwete lina DOSARI, sijui ndio mitindo ya kukopiana hawa vijana viongozi wetu mambo leo? Hata Gadaffi, mtoka Maghreb alikua anatambua mabakia ya ukuloni ki mila na tamaduni zetu asilia.

Chapisha Maoni