POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA MASHABIKI WENYE HASIRA

♠ Posted by Unknown at 11:50
 
Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'.
Stuttgart, Ujerumani
USIKU wa Jumamosi ya Agosti 30 mwaka huu majira ya saa 10 alfajiri, Mwanamuziki Nyota wa Bongo Flava, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya mashabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri shooo ya staa huyo.
Muonekano ndani ya ukumbi mjini Stuttgart, Ujerumani baada ya vurugu kutokea.

Mashabiki hao waliokuwa wamelipia tiketi kwa Euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa shoO ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake Mr. Awin Williams Akipomiemie raia wa Nigeria anayejiita kama Britts Event.
Hapo ndipo mashabiki hao walioona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake.
Kilichowakera zaidi mashabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja vyombo vya muziki huku ma-Djs wakishambuliwa ambao kwa sasa wapo hospitali.
Moja wa Djs hao alipoteza Laptop yake, mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, mashabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee ambaye yupo hoi.
Polisi nchini Ujerumani wamesema tukio hilo la aibu halijawahi kutokea, kwani msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari sana kwani mashabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promota huyo raia wa Nigeria, ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana kujihusisha na mtandao fulani wa biashara haramu.

0 comments:

Chapisha Maoni