WAIMBAJI BONGO WENGI HAWAJUI KUCHEZA ALA ZA MUZIKI

♠ Posted by Unknown at 16:36


                                  
Na  Ammy Nando
FANI  ya sanaa hapa Bongo imekuwa ya ajabu sana.  Si kejeli wala nini, ni mawazo binafsi ningependa kuchangia.  Wengi wetu tumeigeuza sanaa kuwa mahali pa
kujiegemea na kujitafutia riziki, lakini kati yetu wangapi tunaijua vema sanaa hii? Sanaa ambayo inakua kwa kasi kila kukicha.
Je, ni wasanii wangapi maarufu wanajua kucheza vyombo vya muziki.  Kwa mfano, Ben Pol anajua kutumia piano? Je, Diamond anajua kutumia gitaa?
Wengi wetu tumekurupushwa kujiunga na sanaa kutokana na muonekano ama kipaji binafsi cha kujiendeleza.   Kama shule au chuo cha sanaa vingekuwepo tungeweza kukuza upeo wa msanii chipukizi wa muziki kwa kuanza kujua vifaa vya muziki kabla hajatoka rasmi kisanii.
Kwa wasanii wa movie,  je ni wangapi wanajua jinsii ya kuandika  miswada ya filamu (script) au kushika kamera kwa ufasaha? Mambo ni yaleyale, elimu ya sanaa bado adimu kupatikana  na ndiyo maana wengi wetu tunaishia ‘kutesa kwa zamu’.
Waheshimiwa au mataijiri mbona mnatunyonya nguvu bila ya kutuendelezea vipaji vyetu? Nyie hamuoni darasa au shule ya sanaa itakuza sanaa hii tunayoipa kipaumbele kutokana na mafanikio walioyapata kina Profesa Jay, Lady Jay Dee na wengine kibao.
Hivi kila msanii mkongwe akiamua kufanya semina au darasa la kufundishia watu juu ya mambo walioyapitia, hatuwezi kuona jinsi pengo la dhuluma linavyopungua?

Wasanii wenzangu, tafadhalini,  tuchangiane mawazo na kuwaelimisha watakaopenda kuingia kwenye sanaa hii ili kuwafungulia njia mbadala  na si lazima wapitie tulipopitia sisi.  Au unaonaje?

                                     Posted by Mr.Prime on August 22, 2014

0 comments:

Chapisha Maoni