♠ Posted by Unknown at 05:42
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe (kulia)
akimkabidhi Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya
na Ustawi Dkt. Elias Chinamo moja ya kifaa (kamera) itakayotumika kupima
dalili za ugonjwa wa Ebola kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia
viwanja vya ndege ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa
kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
Mkurugenzi
wa Ugavi wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD),Heri Mchunga
(kushoto) akimpima Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara
ya Afya na Ustawi Dkt. Elias Chinamo (kulia) kuonyesha namna moja ya
kifaa cha kupimia joto la mwili wa Binadamu kinavyofanya kazi kwa
kubaini dalili za Ugonjwa wa Ebola eneo la uwanja wa ndege wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Moja
ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za
ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege. Kifaa hicho kina uwezo wa
kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda , joto la msafiri, tarehe
aliyoingia nchini pia uwezo wa kupata takwimu kutoka kwenye hali ya
majimaji au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake.




0 comments:
Chapisha Maoni