SANDRA: NACHUKIA UKE WENZA

♠ Posted by Unknown at 05:56


                                       
Stori: Rhoda Josiah
MKONGWE kwenye sanaa Bongo, Salama Salmin ‘Sadra’ amesema kuwa hakuna kitu anakichukia maishani kama uke wenza.

 
Mkongwe kwenye sanaa ya maigizo Bongo, Salama Salmin ‘Sandra’.
Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili, Sadra ambaye tayari ni mke wa mtu, alisema anajiamini kwa kila jambo ambalo analifanya katika maisha yake na hayupo tayari kukubali kabisa suala la uke wenza kwani anapenda awe peke yake.
“Sipendi uke wenza ingawa dini ninayoiamini (uislamu) inaruhusu na ninamuomba Mungu jambo hilo lisinikute ili niendelee kufurahia maisha yangu ya ndoa,” alisema Sadra.

                                         Posted by Mr.Prime on August 23, 2014

0 comments:

Chapisha Maoni