Mshambulizi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 36 aliwahi kushinda
mataji 10 akiwa stamford Bridge kuanzia mwaka wa 2004-2012 kabla ya
kuguria Galatasaray.
"Nikifaulu kumrejesha Uingereza jambo ambalo natumai litafanyika kwa
haraka ,itakuwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kikosi na
timu kwa jumla''.Mourinho alidhibitisha kuwa The Blues inatafakari
kurejea kwake Uingereza na kuwa anatumai uhamisho huo utatekelezwa bila
hisia kali .
Drogba, alijiunga na Chelsea mwaka wa 2004 akitokea Marseille katika uhamisho ulioigharimu klabu hiyo pauni milioni £24.
Wakati huo aliiongoza Chelsea kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya
Uingereza mataji 4 ya FA , mataji mawili madogo ya ligi mbali na ubingwa
wa bara Ulaya .

Drogba akiwa Galatasaray.
Aliondoka Stamford Bridge mwaka wa 2012 baada ya kutinga penalti
iliyoisaidia klabu hiyo kutwaa kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya
Bayern Munich .
Drogba aliwahi kuichezea klabu ya China Shanghai Shenhua, kabla ya kuijunga na Galatasaray January 2013
0 comments:
Chapisha Maoni