♠ Posted by Unknown at 05:21
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na masheikh
wa mikoa na maimamu wa misikiti katika ukumbi wa bwalo la maafisa wa
Polisi wakati
wa kikao cha muendelezo wa kampeni ya familia yetu haina
mhalifu kilichoratibiwa na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka. Picha
na Hassan Mdeme- wa Jeshi la Polisi
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiwa na Mufti na Sheikh
mkuu wa Tanzania Shabani Simba na viongozi wengine wa dini ya kiislamu
wakati wakiingia katika ukumbi wa bwalo la maafisa wa Polisi kuhudhuria
kikao cha muendelezo wa kampeni ya familia yetu haina mhalifu
kilichoratibiwa na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka.
Viongozi wa dini wametakiwa kuendelea
kufanya doria za kimwili na kiroho katika kuimarisha ulinzi na usalama
ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwajenga vijana katika maadili
mema na kuacha kutenda dhambi ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu
alipokutana na viongozi wa dini ya kiislam katika ukumbi wa Bwalo la
maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es salaam. Kikao hicho
kiliratibiwa na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka inayoongozwa na
Sheikh Issa othuman.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Mufti wa
Tanzania Shabani Simba, Katibu mkuu wa Bakwata, Kadhi Mkuu wa Zanzibar,
Masheikh wa mikoa ya Tanzania bara pamoja Maimamu wa Miskiti.
IGP Mangu alisema kuwa haijawahi kutokea
kokote duniani kwa Polisi kula njama na viongozi wa dini katika
kupambana na wahalifu na watenda dhambi, hivyo aliwaomba viongozi hao
wa dini waongeze mahubiri yenye kuwataka waumini kutenda mema pamoja na
kuongeza nguvu ya kuimarisha kamati za ulinzi na usalama katika nyumba
za kuabudia.
Naye, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania
Shaban Simba alisema kuwa dini zote zinahimiza waumini wake kutenda
mema na kujiepusha kushiriki katika vitendo viovu, hivyo ameliomba Jeshi
la Polisi kuendelea kuwakamata wale wote watakaobainika kutenda uhalifu
kwani hivi sasa uhalifu upo hata kwenye taasisi za dini.
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa mkoa wa
Arusha Shabani Juma, wakati akitoa salamu za mkoa huo, alisema kuwa mkoa
wa Arusha kwa sasa hivi upo shwari na wa amani, hivyo ni wajibu wetu
kulinda amani tuliyonayo kwani ndio msingi wa kila kitu.
Kikao hicho ni muendelezo wa mkakati wa
Jeshi la Polisi katika kuwajengea uwezo viongozi wa dini, ambapo
viongozi hao wa dini waliazimia kwa pamoja kuendelea kushirikiana na
Jeshi la Polisi katika kampeni ya kutengeneza familia zisizo na wahalifu
kupitia mahubili yao pamoja na kuendelea kuimarisha kamati za ulinzi na
usalama katika nyumba za ibada kwa rahisi ya mawasiliano katika
kuwadhibiti wahalifu.


0 comments:
Chapisha Maoni