♠ Posted by Unknown at 07:29
Man united yamnunua Di Maria
Post by Mr.Prime 26 Agosti, 2014
Manchester United imekubali
kumchukua Winga wa Real Madrid Anji di maria kwa pauni milioni 59.7
nakuvunja rekodi ya kiwango cha fedha kwa wachezaji wanaonunuliwa
kuchezea timu za England.
Di Maria mwenye umri wa miaka 26, yuko jijini Manchester na anatarajiwa kufanya vipimo vyake vya kiafya asubuhi hii.Mchezaji huyo pengine ataungana na kikosi cha Man United katika mchezo wa ligi kuu ya England utakaofanyika siku ya jumamosi dhidi ya Burnley
Kitita kilichotolewa kwa ajili ya Muajentina Di Maria kimezidi kiwango cha pauni milioni 50 ambacho kilitolewa na Chelsea kumnyaka Fernando Torres mwaka 2011.
Manchester United imeshawanunua wachezaji kama beki wa kushoto Luke Sho,Kiungo wa kati Ander Herrera na Muajentina Marcos Roho kwa jumla ya Pauni milioni 72 kipindi hiki cha majira ya joto.

0 comments:
Chapisha Maoni