♠ Posted by Unknown at 01:08
Stori: Mwandishi WetuRAPA mwenye jina kubwa katika Bongo Fleva, Rashid Makwiro maarufu kama Chid Benz, amekiri kutoa machozi wakati wa mahojiano redioni baada ya kupatwa na hisia kali, akikumbuka mambo mbalimbali ya maisha.
Rapa mwenye jina kubwa katika Bongo Fleva, Rashid Makwiro maarufu kama Chid Benz (kushoto) akiwa na 'Diamond'.
“Nilikuwa namzungumzia Diamond, alinikumbusha mambo mengi, ni mchapakazi, anajituma na amejipanga, anajua alikotoka na anathamini alipopitia, nikajikuta nimepatwa na ‘emotions’ zilizonitoa machozi,” alisema msanii huyo aliyetoa kazi mpya hivi karibuni.Wimbo huo mpya unaokwenda kwa jina la Mpaka Kuchee, ameufanya baada ya kukaa kimya kwa muda wa mwaka mmoja, kiasi cha kuleta hisia kuwa huenda amekwisha makali yake. Kibao hicho amewashirikisha wakali wengine, mkongwe AY na msanii aliye juu kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’.




0 comments:
Chapisha Maoni