Mchepukoleo

NINGEKUWA MIMI NYALANDU, NISINGETANGAZA KUGOMBEA URAIS

♠ Posted by Unknown


Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samuel Nyalandu.
Kwako Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samuel Nyalandu.
Najua uko bize sana kwa sasa ukiweka sawa mipango yako kuhakikisha mwaka huu unaingia ikulu katika uchaguzi mkuu ujao, najua itakuwa vigumu kwa ‘kapuku’ kama mimi kuonana na wewe ndiyo maana nimeamua kutumia ukurasa huu kufikisha ujumbe wangu kwako.
Mheshimiwa, mimi sikuzaliwa Agosti 18, 1970 kama wewe wala sijawahi kusoma Shule ya Msingi Pohama, Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha wala sijawahi kusoma Shule ya Sekondari ya  Illboru na kuhitimu kidato cha sita kama wewe.
Sijawahi kusoma vyuo mbalimbali duniani kama University of Buckingham cha Uingereza, Wartburg College na Waldorf College, vyote vya Marekani kama wewe. Sijui chochote kuhusu uongozi wala siasa, niponipo tu, kapuku nisiye na mbele wala nyuma.
Hata hivyo, ningekuwa mimi katika nafasi yako, walahi nakuapia nisingepaza sauti yangu na kutangaza kwamba nataka kugombea urais kama ulivyofanya wewe hivi karibuni Katika Uwanja wa Ilongero, kwenye jimbo lako la Singida Kaskazini.
Najua ni haki yako ya msingi kugombea kama ilivyo kwa Mtanzania mwingine yeyote lakini nakuhakikishia, kama ungepata nafasi ya kujitathmini wewe kwanza, kuangalia udhaifu mkubwa uliouonesha tangu ulipokuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii hadi sasa ukiwa waziri kamili katika Wizara ya Maliasili na Utalii, usingethubutu kutangaza nia.
Mheshimiwa, umesahau jinsi ulivyokumbwa na kashfa kibao za kudaiwa kushirikiana na kampuni za kigeni za utalii na uwindaji kuihujumu serikali kwa kujenga mazingira ya kukwepa kodi?
Umesahau jinsi ulivyohusishwa na kampuni ambayo inadaiwa una mgongano nayo wa kimaslahi ya Ahsante Tours, ikidaiwa ulishinikiza kampuni hiyo isamehewe mamilioni ya kodi mpaka TANAPA walipoikomalia ndiyo kodi ikalipwa?
Mheshimiwa, umesahau jinsi ulivyoidhinisha ununuzi wa helikopta chakavu eti kwa ajili ya kukabiliana na ujangili, mwisho helikopta hiyo ikaanguka na kusababisha vifo vya marubani wetu wanne hivi karibuni?
Mheshimiwa, umesahau jinsi nchi yetu ilivyoingia kwenye doa kubwa kufuatia ujangili wa kupindukia na biashara ya meno ya tembo ilivyoshamiri kwa sababu ya wewe na wenzako kushindwa kutimiza majukumu yenu kwa umakini?
Vipi kuhusu marekebisho ya hovyo ya sheria ya uwindaji unayoshikia bango kwamba kipindi cha uwindaji kiongezwe kutoka muda wa miezi sita hadi tisa kwa manufaa ya wawindaji bila kujali uhifadhi na kuzaliana kwa wanyama wetu?
Madudu ambayo kwa namna moja au nyingine umekuwa ukidaiwa kuhusika nayo, ni mengi mno. Nikisema nitaje mojamoja, nitayajaza ukurasa mzima.
Hapana mheshimiwa, utendaji wako katika sehemu zote ulizopita, hauridhishi. Umekuwa ukionekana ‘mzigo’ kila unapopita achilia mbali jimboni kwako ambako kuna ahadi kibao ulizitoa wakati wa kampeni lakini mpaka sasa hujazitimiza.
Kama kuongoza jimbo lako la Singida Kaskazini na kuongoza wizara moja tu kumekushinda, utaweza kuongoza nchi? Ikulu ni mahali patakatifu mheshimiwa, waachie wenye uwezo watangaze nia ya kugombea lakini siyo wewe.
Wasalaam.

MARTIN,AUNT WAZUA UTATA!

♠ Posted by Unknown in
MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda na mwigizaji Aunt Ezekiel wamenaswa chobingo wakiwa katika pozi tata.Tukio hilo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Klabu ya 71, Tegeta-Kibaoni jijini Dar kulipokuwa na shoo ya kuukaribisha mwaka iliyoandaliwa na Kampuni ya Endless Fame.

URAIS 2015: NYALANDU AKESHA AKICHEZA SEBENE!

♠ Posted by Unknown in

WAZIRI wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais wa nchi amefanya kufuru kubwa katika Kanisa la Efatha linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira, mjini Kibaha, Pwani baada ya kusakata sebene la Injili usiku wa manane.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiselebuka.

WEMA AUZA GARI LA DIAMOND

♠ Posted by Unknown in

Lile gari jipya aina ya Nissan  Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limezua mapya ambapo baada ya kudai linamchefua sasa anadaiwa kuwa analiuza kwa kigezo kwamba hataki gundu mwaka huu mpya wa 2015.
Gari jipya aina ya Nissan  Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’

PANYA ROAD WATIKISA JIJI LA DAR

♠ Posted by Unknown in
Muonekano wa jiji la Dar es Salaam (Picha na Maktaba).
KIKUNDI kinachodaiwa kuwa Panya Road kimetikisa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi.

Mwanamfalme ahusishwa na unyanyasaji UK

♠ Posted by Unknown in

Mwanamfalme Andrew

Kasri ya Buckingham imepinga madai kwamba mmoja ya wana wa malkia Elizabeth mwanamfalme Andrew amekuwa alijihusisha katika tabia mbaya baada ya kubainika kwa nakala za mahakamani nchini Marekani zinazomuhusisha na madai ya unyanyasaji wa kijinsia.

UN:Itachukua mda mrefu kuangamiza Ebola

♠ Posted by Unknown in

Kiongozi wa ujumbe wa ebola katika shirika la Umoja wa Mataifa Tony Banbury

Kiongozi wa ujumbe wa ebola katika shirika la Umoja wa Mataifa amesema kuwa harakati za kukabiliana na ugonjwa huo zinazochukuliwa hazijafikia kiwango cha kuuangamiza katika eneo la Afrika Magharibi.

Steven Gerrard kuihama Liverpool

♠ Posted by Unknown in


Steven Gerrard nahodha wa klabu ya Liverpool

Nahodha wa timu ya Liverpool ya Uingereza Steven Gerrard ataondoka katika klabu hiyo wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mancity yafika kileleni mwa ligi ya EPL

♠ Posted by Unknown in

Manchester City yafika katika kilele cha uongozi wa ligi ya EPL baada ya kuishinda Sunderland 3-2

Mchezaji Frank Lampard alifunga bao la ushindi kupitia kichwa chake dhidi ya Sunderland na kuiweka Manchester City sawa na Chelsea katika kilele cha ligi ya Uingereza.

Chelsea yapewa kichapo na Totenham

♠ Posted by Unknown in

Waasi nchini DRC Congo

Makataa yaliotolewa na mataifa ya maziwa makuu pamoja na jamii ya kimataifa kwa wapganaji wa Hutu nchini Rwanda FDLR kusalimisha silaha zao yanakamilika hii leo siku ya ijumaa.

Makataa ya FDLR kujisalimisha yakamilika

♠ Posted by Unknown in

Waasi nchini DRC Congo

Makataa yaliotolewa na mataifa ya maziwa makuu pamoja na jamii ya kimataifa kwa wapganaji wa Hutu nchini Rwanda FDLR kusalimisha silaha zao yanakamilika hii leo siku ya ijumaa.

Idara ya polisi yaongoza kwa ufisadi TZ

♠ Posted by Unknown in

Jeshi la polisi nchini tanzania ndio taasisi fisadi zaidi chini humo

Idara ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.